Gossip

Azeezah Hashim Asema Wanaume Wanaomfuata Andrew Tate au Kibe ni Red Flag

Azeezah Hashim Asema Wanaume Wanaomfuata Andrew Tate au Kibe ni Red Flag

Mtangazaji na mrembo maarufu Azeezah Hashim amezua gumzo mitandaoni baada ya kueleza msimamo wake kuhusu wanaume wanaoamini na kufuata mitazamo ya wanablogu wenye utata Andrew Tate na Andrew Kibe.

Katika mahojiano na Milard Ayo, Azeezah alisema wazi kuwa hawezi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume anayeshikilia imani kwamba wanaume na wanawake hawawezi kuwa marafiki au wenza wa kweli. Alisisitiza kuwa uhusiano bora hujengwa kwa heshima, maelewano, na upendo wa kweli si kwa nguvu au ubabe wa kijinsia.

“Mimi nahitaji mwanaume ambaye anaonyesha upendo wa kweli, siyo mtu anayefikiri kwamba wanawake ni wa kutumia au wa kuwatawala. Ukiniambia unaamini itakadi kama za Andrew Tate au Kibe, hiyo ni red flag ya kwanza na ya mwisho,” alisema Azeezah kwa msisitizo.

Kauli hiyo imezua mijadala mitandaoni huku baadhi ya watu wakimpongeza kwa kusimamia maadili ya heshima kwenye mahusiano, huku wengine wakikosoa mtazamo wake wakidai kila mtu ana uhuru wa kufuata kile anachoamini.

Andrew Tate na Andrew Kibe ni majina yanayojulikana kwa kutoa mitazamo mikali kuhusu jinsia, ambayo kwa sehemu kubwa imekuwa ikipingwa na watu wanaotetea usawa wa kijinsia.