
Ronald Fenty, baba mzazi wa nyota maarufu wa muziki wa pop Rihanna, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70. Kwa mujibu wa Starcom Network News kutoka Barbados, Fenty alifariki mapema Jumamosi asubuhi jijini Los Angeles baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Ingawa chanzo rasmi cha kifo chake hakijatangazwa, ripoti zinaeleza kuwa wanafamilia wake walikusanyika California kwa ajili ya kumuenzi na kuomboleza kifo chake. Hadi sasa, Rihanna hajatoa tamko lolote rasmi kuhusu kifo cha baba yake.
Taarifa za msiba huu zimekuja wakati Rihanna akiwa mjamzito na anatarajia mtoto wake wa tatu na mpenzi wake, rapa ASAP Rocky.