
Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Ruth K, amefunguka baada ya kupoteza simu yake aina ya iPhone 14 jana katika uwanja wa Kasarani wakati wa mechi ya michezo ya CHAN 2024 kati ya Zambia na Harambee Stars.
Kupitia mitandao ya kijamii, Ruth K amesema simu hiyo iliibiwa katikati ya shamrashamra za mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani kushuhudia pambano hilo. Ameomba msaada wa umma na kutangaza kuwa yuko tayari kutoa zawadi ya KSh 30,000 kwa yeyote atakayesaidia kurudisha simu hiyo.
Ruth K amesisitiza kuwa kilicho na thamani zaidi kwake ni kumbukumbu na taarifa binafsi zilizohifadhiwa kwenye kifaa hicho, kuliko simu yenyewe. Taarifa hiyo imezua gumzo mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimfariji huku wengine wakionya mashabiki kuwa makini zaidi wanapohudhuria hafla zenye umati mkubwa wa watu.