
Muigizaji maarufu wa Kenya, Tyler Mbaya, almaarufu Baha, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu namna uvujaji wa video zake za faragha ulimsaidia kuimarisha kujiamini kwake binafsi.
Akizungumza na mtangazaji Prince Newton, Tyler alisema kuwa tukio hilo lilikuwa la kushangaza, lakini lilimfungua macho na kumuondolea woga wa kuhukumiwa na watu.
“Sasa naingia mahali kwa ujasiri. Hata naweza kucheka nikijiuliza kama Mama Mboga aliona hizo video,” alisema kwa ucheshi.
Ingawa tukio hilo lilikuwa na changamoto zake, Tyler alikiri kuwa halimsumbui tena, lakini anajiandaa kwa siku ambayo binti yake, Astra, atauliza kuhusu hilo.
“Najua siku moja atakua na kuuliza maswali, kwa hivyo lazima nijue nitamweleza nini,” alisema kwa ukweli.
Mashabiki wake wamechangia maoni tofauti, baadhi wakimsifu kwa ujasiri na uwazi wake, huku wengine wakikumbusha umuhimu wa faragha na maadili hasa kwa watu maarufu wenye familia.
Tyler Mbaya, ambaye alijizolea umaarufu kupitia kipindi cha Machachari, amekuwa mstari wa mbele kushiriki safari yake ya maisha, changamoto na mafanikio yake na mashabiki, huku akisisitiza umuhimu wa kujikubali hata wakati jamii inakutazama kwa jicho la hukumu.