Entertainment

Bahati Aachwa na Maswali Mengi Baada ya Mwanamke Kujitokeza Akidai Kumzaa

Bahati Aachwa na Maswali Mengi Baada ya Mwanamke Kujitokeza Akidai Kumzaa

Staa wa muziki nchini Kenya, Bahati, amejikuta katika hali ya huzuni na mshtuko mkubwa baada ya mwanamke mmoja kujitokeza mtandaoni akidai kuwa ndiye mama yake halisi, licha ya mama mzazi wa Bahati kufariki miaka mingi iliyopita wakati akiwa bado mtoto mdogo.

Katika video aliyochapisha mitandaoni, Bahati ameeleza kuwa kifo cha mama yake alikishuhudia akiwa na umri wa takriban miaka saba, na hata kuhudhuria mazishi yake. Amesema kuwa maisha yake yote amekuwa na kumbukumbu hiyo wazi, jambo linalomfanya kushindwa kuelewa madai ya mwanamke huyo.

Bahati ameonesha kuchanganyikiwa na kutokuwa na uhakika kuhusu hatua anazopaswa kuchukua. Ameeleza kuwa hana mawasiliano na mwanamke huyo, na hata hajui pa kuanzia ili kuthibitisha madai hayo.

Amehoji pia kama inawezekana kufanyika uthibitisho wa DNA baada ya kifo cha mama yake na kusisitiza kuwa kama kweli mama yake angekuwa hai, hilo lingekuwa jambo la furaha isiyo na kifani maishani mwake.

Msanii huyo, ambaye mara nyingi huonekana mchangamfu na mwenye utani, amesema kuwa suala hilo limemgusa kwa kina na kumwacha katika hali ya huzuni na maswali mengi bila majibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *