Entertainment

BAHATI ADOKEZA UJIO WA KOLABO YAKE NA ALI KIBA

BAHATI ADOKEZA UJIO WA KOLABO YAKE NA ALI KIBA

Msanii wa muziki nchini Bahati Kenya’ amethibitisha kukamilika kwa kolabo yake na Staa wa muziki nchini Tanzania, Ali Kiba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bahati amepost picha ya pamoja na King Kiba kwa kusema kwamba kolabo yake na hitmaker huyo wa ngoma ya “Utu” ni moto wa kuotea mbali huku akiwaachia mashabiki swali kama wako tayari kwa ajili ya video ya ngoma hiyo.

“BREAKING NEWS  @Officialalikiba  @BahatiKenya Collabo Done  Kenya/ Tanzania I swear this is Big My Boss @Joho_001 Can Confirm this!  ARE YOU READY FOR THE MUSIC VIDEO??? ” Aliandika Bahati.

Hata hivyo Bahati hajaweka wazi kolabo yake hiyo itatoka lini ila itakuwa kazi yake ya kwanza kuachia mwaka wa 2022  na ya tatu kufanya na msanii wa Bongofleva ikizingatiwa kipindi cha nyuma alifanya kolabo na Aslay pamoja na Rayvanny.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *