Entertainment

BAHATI AFUNGUKA KUVAMIWA NA MAJANGILI KUMSHINIKIZA AJIONDOE UBUNGE MATHARE

BAHATI AFUNGUKA KUVAMIWA NA MAJANGILI KUMSHINIKIZA AJIONDOE UBUNGE MATHARE

Msanii aliyegeukia siasa Bahati amedai kuwa mpenzi wake Antony Oluoch alimtumia majangili kumtishia maisha ili ajiondoe kwenye azma yake ya ubunge Mathare

Kupitia mitandao yake ya kijamii Bahati amesema vijana hao ambao sio wakaazi wakaazi alimvamia na kumpiga kiasi cha kurarua shati lake la chama chake cha Jubilee huku wakimtishia kuwa wataangamazia kama atajiuzulu kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema mpinzani wake huyo amejaribu kila njia kuzima ndoto yake lakini amesema kidete kwa ajili ya watu wa Mathare ambao wamehangaika kwa muda mrefu.

Hata hivyo amepuzilia mbali shinikizo za kutaka kujiondoa kwenye ubunge Mathare huku akidai kuwa atakuwa kwenye debe Agosti 9 ambapo akiwarai wakaazi wa mpe kura kwa wingi licha ya vitisho anavyozidi kupokea kila kuchao.

Kauli ya Bahati imekuja mara baada ya Raila Odinga kuahidi kumpa kazi kwenye serikali yake na kumtaka ampe nafasi Mbunge wa sasa wa Mathare Athony Oluoch kutetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *