Entertainment

Bahati Aingia Kwenye Orodha ya Wasanii Wenye Nyimbo Zilizopata Ukosoaji Mkubwa YouTube

Bahati Aingia Kwenye Orodha ya Wasanii Wenye Nyimbo Zilizopata Ukosoaji Mkubwa YouTube

Msanii wa muziki wa Kenya, Bahati, amejiunga na orodha ya wasanii waliokumbwa na ukosoaji mkubwa kwenye jukwaa la YouTube baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya “Seti”.

Video hiyo, iliyoachia rasmi Jumatano wiki hii, imepokea zaidi ya dislikes 24,000 dhidi ya takribani likes 16,000, hali inayoashiria mapokezi yenye sura hasi kutokana maudhui yake yanayodaiwa kuhamasisha ngono katika jamii.

Kwa matokeo haya, Bahati sasa anajiunga na Vera Sidika, ambaye wimbo wake “Popstar” ulipata zaidi ya dislikes 28,000 dhidi ya likes 13,00 , pamoja na Willy Paul, ambaye bado anashikilia rekodi kupitia kibao chake “Lamba Nyonyo” kilicho na zaidi ya dislikes 38,000 dhidi ya likes takribani 5,300 pekee.

Hata hivyo, Bahati hajatoa kauli rasmi kufuatia ukosoaji unaoendelea dhidi ya “Seti”. Mashabiki wamegawanyika, baadhi wakimtetea kwa ubunifu wake, huku wengine wakihisi kwamba msanii huyo amepoteza mwelekeo na heshima ya muziki wake wa awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *