Entertainment

Bahati Akanusha Kutumia Sakata la Mwanamke Aliyedai ni Mamake kuwa Kiki

Bahati Akanusha Kutumia Sakata la Mwanamke Aliyedai ni Mamake kuwa Kiki

Msanii wa muziki nchini Keny, Bahati, amekanusha madai kwamba anatumia sakata la mwanamke aliyejitokeza akidai ni mama yake mzazi kama mbinu ya kujipatia umaarufu mitandaoni.

Bahati amesema tukio hilo limemshangaza kwa kuwa halikuwa sehemu ya mipango yake ya kujipatia kiki. Amefafanua kwamba mwanamke huyo amekuwa akimtafuta kwa zaidi ya miaka mitano, na hata aliwahi kuwasiliana na ndugu yake mkubwa bila mafanikio.

Msanii huyo, ameeleza kuwa alimwona mwanamke huyo kwa mara ya kwanza kupitia video iliyosambaa mtandaoni, akisema kuwa ingawa baadhi ya mashabiki mitandaoni wanachukulia sakata hilo kama mzaha, kwake binafsi ni jambo lenye uzito.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hajawahi kupanga au kutumia hali hiyo kama njia ya kujipatia umaarufu, bali analichukulia kama tukio la maisha ambalo limemgusa kwa undani ikizingatiwa kuwa mama yake mzazi alifarikia miaka nyingi iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *