Mwanamuziki Bahati amemchana bila huruma Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Nchini (FKF), McDonald Mariga, akidai kwamba hana jina kubwa la kutumiwa kama chanzo cha kiki.
Bahati amesema anamuheshimu Mariga kama gwiji wa soka, lakini akashangazwa na madai kwamba anatafuta umaarufu kupitia jina lake. Amesisitiza kuwa hata binti yake wa mwisho, Malaika, ana umaarufu mkubwa zaidi ukilinganisha na Mariga.
Msanii huyo pia ameongeza kuwa kulikuwa na hujuma nyingi dhidi yake kufanikisha mchakato wa kutoa ahadi yake ya shillingi millioni moja kwa Hatambee stars. Kwa mujibu wa maneno yake, waliopanga wanajua ukweli.
Kauli hizo zimezua gumzo kubwa, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema ana haki ya kulinda heshima yake, na wengine wakimtaka aendelee kuheshimu wachezaji waliowahi kuitumikia Kenya.