
Staa wa muziki nchini Bahati amefunguka sababu za kudinda kuchukua kazi ambayo kinara wa Azimio Raila Odinga aliahidi kumpa pindi atakapotua uongozi wa nchi kwenye uchaguzi uliokamilika.
Bahati amesema alijua kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ungekumbwa na dosari na ndio maana akaendelea na azma yake ya kuwania ubunge Mathare licha ya kushurutishwa kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.
Katika hatua nyingine Hitmaker huyo wa “”Adhiambo anaamini kuna siku jamii ya Kamba itamtoa rais ambaye ataongoza taifa la Kenya licha ya Odinga kumtumia vibaya Kalonzo Musyoka ambaye alikuwa na nyota ya kuiongoza jamii hiyo.
Hata hivyo Bahati ambaye amesisitiza kuwa atakuwa kwenye kinyanganyiro cha urais mwaka 2037 amejinasibu kuwa hajutii kitendo cha kukosa ubunge Mathare kwa kuwa yeye ni moja kati ya watu ambao wapo ndani ya serikali.