Entertainment

Bahati Ampongeza Jux Kwa Kuiwakilisha Afrika Kimuziki, Azua Tetesi za Wimbo Mpya

Bahati Ampongeza Jux Kwa Kuiwakilisha Afrika Kimuziki, Azua Tetesi za Wimbo Mpya

Staa wa muziki nchini Kenya, Bahati, amempongeza nyota wa Bongo Fleva Jux kwa mafanikio makubwa anayoyapata kimuziki, akisema kuwa ushindi wake ni baraka kwa Afrika na pia chanzo cha shinikizo kwa wasanii wengine kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Kupitia mitandao ya kijamii, Bahati ameeleza kufurahishwa na jinsi Jux anavyopeperusha bendera ya Afrika katika anga ya kimataifa, akibainisha kuwa mafanikio hayo yanaweka viwango vipya kwenye tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, kilichozua gumzo zaidi ni video aliyoposti Bahati akiwa pamoja na Jux katika mazingira yanayofanana na ya harusi. Katika video hiyo, wawili hao wanaonekana wakiwa wamepambika vizuri, hali iliyowafanya mashabiki wengi kuamini kuwa huenda walikuwa wakishoot video ya wimbo wao mpya.

Tetesi hizo zilipata nguvu zaidi baada ya caption ya Bahati iliyoambatana na video hiyo, ambapo aliandika maneno yaliyoashiria mashabiki waendelee kusubiri, jambo lililowafanya wengi kuamini kuwa ngoma mpya iko njiani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *