Gossip

Bahati Aomba Ulinzi Baada ya Majambazi Kuvamia Nyumba Yake

Bahati Aomba Ulinzi Baada ya Majambazi Kuvamia Nyumba Yake

Msanii wa muziki, Bahati, ameibua taharuki baada ya kudai kwamba nyumba yake ilivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha mapema alfajiri.

Kwa mujibu wa Bahati, tukio hilo lilitokea kati ya saa 10:27 alfajiri na saa 11:30 asubuhi, na kuacha familia yake katika hali ya hofu. Ameeleza kuwa uvamizi huo umetokea siku chache tu baada yake na mkewe, Diana Marua, kuonyesha hadharani mafungu ya pesa taslimu yenye thamani ya mamilioni wakiwa ndani ya nyumba yao, jambo ambalo huenda liliwavutia wahalifu.

Kupitia mitandao ya kijamii, Bahati ameeleza kuwa ana hofu kubwa kuhusu usalama wa familia yake na sasa ameomba moja kwa moja Inspekta Jenerali wa Polisi kuingilia kati na kutoa ulinzi wa haraka.

Tukio hilo limekuja saa chache tu baada ya Bahati kuwatolea uvivu wakosoaji wake waliodai ameshindwa kutimiza ahadi ya kutoa shilingi milioni moja. Akizungumza jana akiwa na msanii DK kwenye Beat, Bahati alionekana akibeba shilingi milioni tatu taslimu, akisisitiza kwamba ana utajiri mkubwa na hawezi kushindwa na jambo dogo kama hilo.

Hata hivyo, hatua yake ya kuonyesha mafungu ya pesa taslimu nyumbani huenda ikawa imewachochea wahalifu waliovamia makazi yake..

Tukio hili limezua gumzo mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wamemlaumu kwa kuonyesha utajiri wake hadharani, huku wengine wakimuonea huruma na kushinikiza mamlaka kuchukua hatua za haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *