
Msanii kutoka Kenya, Bahati, ameibuka na kuwatolea uvivu wakosoaji wanaomshutumu kwa tabia yake ya kuonyesha mali na maisha ya kifahari kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa msanii huyo, hakuna tatizo lolote katika kuonyesha mafanikio kwani ameyapata kupitia juhudi kubwa na bidii aliyoweka kwa muda mrefu. Anasisitiza kuwa kila mtu ana uhuru wa kuishi maisha anayoyataka na kwamba mafanikio yake ni kielelezo cha kazi ngumu, uvumilivu na imani.
Bahati ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea kufurahia maisha na kutumia jukwaa lake kuonyesha baraka alizopewa na Mungu, sambamba na mipango ya miradi mikubwa ya muziki na biashara anayotarajia kuzindua siku za usoni.
Katika sikiu za hivi karibuni, Bahati amekuwa gumzo baada ya kushiriki picha na video akionekana na fedha taslimu, magari ya kifahari na maisha ya kifamilia yenye mvuto.