
Mwanamuziki aliyegeukia siasa, Bahati amewajibu kitaalamu wanaomubeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupoteza kiti cha ubunge Mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika majuzi nchini Kenya.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Bahati amesema hatojutia maamuzi yake ya kuwania ubunge Mathare kwa kuwa amejifunza mambo mengi kwenye ulingo wa siasa licha ya kwamba zoezi zima la kuhesabu kura lilikumbwa na dosari.
Hitmaker huyo wa βAdhiamboβ amesema wanaomkosoa kwenye mitandao ya kijamii wanamuonea kijicho kutokana na hatua kubwa aliyopiga maishani.
Utakumbuka baadhi ya mastaa akiwemo Willy Paul walimkejeli Bahati kwa kumpongeza mpinzani wake Anthony Oluoch ambaye ndiye mbunge mteule wa Mathare, kaunti ya Nairobi.