Entertainment

Bahati kufunga ndoa Novemba 30 mwaka huu

Bahati kufunga ndoa Novemba 30 mwaka huu

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Bahati ameashiria kufunga pingu za maisha na mama ya watoto wake Diana B mwishoni mwa mwezi huu.

Bahati amedokeza hayo kwa picha ya kupitia ukurasa wake wa Instagram na kisha kuweka ishara ya pete ya ndoa ambayo ameambatanisha na ujumbe unaotaja tarehe 30/11 kufanya jambo la kihistoria.

“30TH NOVEMBER 2022 ”, Ameandika.

Hata hivyo ujumbe huo umezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wamedai huenda Bahati akahalalisha ndoa yake na Diana B kwa njia ya harusi huku wengine wakihoji ni ujio wa ngoma yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia siku hiyo.

Ikumbukwe kwa sasa Bahati anafanya vizuri na singles zake mbili “My Beginning” na “Mambo ya Mhesh Remix” ambayo amemshirikisha Sosuun pamoja na Ssaru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *