
Mtandao wa Tmz umeripoti kuwa kampuni ya mitindo na mavazi kutokea Paris, Ufaransa imeamua kuvunja ushirikiano katika uzalishaji wa mavazi kati yao na rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West.
“Balenciaga haina mpango wa kuendelea na ushirikiano kati yetu na Kanye West”- Chanzo cha kuaminika kutokea Tmz
Chanzo hicho hakijaweka wazi sababu ya kampuni hiyo kuachana na rapa huyo wakati wiki kadhaa zilizopita Kanye alikuwa mmoja wa washiriki katika onyesho kubwa la mavazi ya kampuni hiyo huko jijini Paris.