Sports news

Bandari FC Yamtangaza Mohammed Borji Kama Kocha Mpya

Bandari FC Yamtangaza Mohammed Borji Kama Kocha Mpya

Klabu ya Bandari FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya (FKF Premier League) imemtangaza rasmi Mohammed Borji kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Ken Odhiambo aliyeondolewa majukumu yake wiki iliyopita.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Bandari FC ilifichua kuwa Borji ambaye ni raia wa Morocco na aliwahi kuchezea klabu ya Wydad Casablanca amesaini mkataba wa mwaka mmoja na ataiongoza timu hiyo kwa msimu huu wa ligi.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Taufiq Balala, alisema kuwa uteuzi wa Borji ni sehemu ya mikakati ya kuipa timu nguvu mpya na kuhakikisha Bandari inakuwa miongoni mwa wagombea wakuu wa ubingwa msimu huu. Borji, kwa upande wake, ameahidi kujenga kikosi imara na chenye ushindani mkubwa, akisema analenga kuona Bandari ikirejea kileleni mwa soka la Kenya.

Kocha huyo mpya atasaidiwa na Tarik Bendamou, pia kutoka Morocco, ambaye atachukua nafasi ya John Baraza kama kocha msaidizi. Borji na Bendamou wataanza rasmi majukumu yao kwenye mchuano wa kwanza dhidi ya AFC Leopards utakaopigwa tarehe 15 Oktoba.

Baada ya raundi tatu za ligi, Bandari FC, waliotwaa taji lao la mwisho mwaka 2015 waliposhinda Kombe la FKF, anashikilia nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *