Entertainment

Barnaba Classic awapa somo wasanii kuhusu nidhamu kwenye kazi zao

Barnaba Classic awapa somo wasanii kuhusu nidhamu kwenye kazi zao

Mwimbaji nyota wa muziki wa Bongofleva, msanii Barnaba Classic amewakumbusha wasanii wenzake kuwa na heshima pamoja na nidhamu kwa watu wengine.

Barnaba ametumia insta story yake kuwatahadharisha wakumbuke kuna kesho..

“Ndugu zangu wasanii tujifunze heshima na kuheshimu mipaka yetu ya kazi kwa kila mmoja. Lakini pia tujifunze kuwa na upendo kweli na kutoleta mashauzi Mbuzi ambayo kuna muda baadhi ya mambo hayahitaji mbwembwe nyingi kuliko busara. Tuwe na hekima wakati mwingine. Sio kama wengine hatujui kuongea ila tumelelewa kwenye busara.” ameandika Barnaba Classic.

“Nimekuwa kwenye huu muziki yapata miaka 18 sasa lakini sijawahi kumdharau anayekuja leo na aliyeanza kabla yangu. Lakini nadhani kuna jambo kubwa najivunia sana katika maisha yangu ya muziki kuishi bila kuzoea watu hata kama nawajua na kuwachukulia poa. Kwa hiyo ndugu zangu wasanii wenzangu, tuwe na nidhamu na mnapofanya mambo ya kuvunja heshima na mipaka muwe mnakumbuka kuna kesho”. amemalizia Barnaba Classic kwenye mfululizo wa jumbe zake kupitia insta story yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *