Entertainment

Barnaba Classic Awataka Wasanii Kusajili Majina Yao ya Kisanii

Barnaba Classic Awataka Wasanii Kusajili Majina Yao ya Kisanii

Msanii wa BongoFleva Barnaba Classic ametoa wito kwa wasanii na wadau wa sanaa nchini Tanzania kuhakikisha wanasajili majina yao ya kisanii pamoja na misemo wanayotumia mara kwa mara, ili kuepuka migogoro ya kisheria inayoweza kujitokeza baadaye.

Akizungumza kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Barnaba amesema wasanii wengi wamekuwa wakichukulia poa suala la usajili wa majina na misemo yao, jambo linalowafanya kujikuta kwenye sintofahamu pindi haki za matumizi ya majina hayo zinapodaiwa kisheria.

Barnaba amesema kumeshuhudiwa matukio ambapo wasanii wamekuwa maarufu kwa majina fulani, lakini baadaye wakazuiwa kuyatumia au kufunguliwa madai kwa sababu hawakuwahi kuyasajili mapema kwa mujibu wa sheria.

Msanii huyo amesisitiza kuwa taasisi kama COSOTA zipo kwa ajili ya kulinda haki za wasanii, lakini akabainisha kuwa jukumu la kwanza ni la msanii mwenyewe kuchukua hatua za kujilinda mapema kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *