Sports news

Bayern Munich Wapeleka Ofa Kwa Nyota wa Arsenal Gabriel Martinelli

Bayern Munich Wapeleka Ofa Kwa Nyota wa Arsenal Gabriel Martinelli

Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani inazidi kuonyesha nia ya kumsajili winga wa Arsenal, Gabriel Martinelli, huku ikichunguza uwezekano wa kuongeza mshambuliaji huyo wa Brazil katika kikosi chake msimu ujao.

Martinelli, aliyekuwa na msimu mgumu wa 2024/25 kutokana na majeraha ya mara kwa mara, alionyesha ubora mkubwa zaidi msimu wa 2022-23, ambapo alifunga mabao 15 katika Ligi Kuu ya England, rekodi bora zaidi ya mchezaji wa Brazil kuwahi kufanikisha katika ligi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti za Ujerumani, Martinelli ndiye mshambuliaji pekee anayehusishwa kwa sasa na mabingwa hao wa Bundesliga, ingawa Bayern pia wamepeleka ofa kwa Nico Williams wa Athletic Club. Wameonesha pia nia ya kumsajili Rafael Leão wa AC Milan.

Mbali na hilo, tetesi pia zinaeleza kwamba Bayern wanaangalia uwezekano wa kupata huduma za wachezaji wawili wa Liverpool, Cody Gakpo na Luis Díaz, kama sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha safu ya ushambuliaji. Hali hii inaonyesha Bayern wanataka kuboresha zaidi kikosi chao kujiandaa na mashindano ya msimu ujao.