Entertainment

BEBE COOL ATAKA KUPAMBANISHWA KIMUZIKI NA JOSE CHAMELEONE

BEBE COOL ATAKA KUPAMBANISHWA KIMUZIKI NA JOSE CHAMELEONE

Kwa muda mrefu, mashabiki wa muziki nchini Uganda wamekuwa wakitamani pambano la muziki kati ya Jose Chameleone na Bebe Cool.

Sasa akiwa kwenye moja ya Interview Bebe Cool, amerithia ombi la mashabiki la kutaka pambano la muziki kati yake na Chameleone kuandaliwa kwa kusema kwamba yupo tayari kushindana na hitmaker huyo wa “Valu valu.”

Bebe cool amedai kwamba yeye na bosi huyo wa Leone Island wana nyimbo nyingi na nguvu za kutosha kuanzisha tamasha kubwa la kuwapambanisha kimuziki.

Bosi wa Gagamel amesema mashindano ya muziki yanafaida kubwa kwa tasnia ya muziki nchini uganda ikizingatiwa kuwa amefaidika pakubwa kushindanishwa na wasanii kama Bobi wine, Radio na Weasel.

Hitmaker huyo wa “Gyenvude” amedai kwamba alishinda mapambano ya zamani ya muziki kwa sababu alifanya utafiti wa kutosha dhidi ya washindani wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *