
Mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amewatolea uvivu waandaji wa tuzo za muziki nchini humo kwa kuwapa wasanii tuzo ambazo hazina muhimu wowote.
Akiwa kwenye moja ya Interview Bebe Cool amesema waandaji wa tuzo nchini Uganda wamekuwa na mazoea ya kuwapa wasanii tuzo ambazo msanii hawezi uuza na akapata pesa za kujikimu kimaisha.
Bosi huyo wa Gagamel amedokeza mpango wa kuja na tuzo yake mwakani na washindi watapokezwa kati ya shillingi laki moja na laki tatu kulingana na kipengele ambacho msanii husika atakuwa ameteuliwa kushiriki.
Kauli ya Bebe Cool imekuja siku chache mara baada ya Spice Diana kuwachana waandaji wa tuzo nchini uganda wasimteue kwenye tuzo zao bila kumshirikisha.