Entertainment

Ben Pol aomba msamaha EX wake Arnelisa kwa kumzungumzia vibaya

Ben Pol aomba msamaha EX wake Arnelisa kwa kumzungumzia vibaya

Msanii wa Bongo Fleva Ben Pol ameandika barua ya wazi kumuomba msamaha aliyekuwa wake Anerlisa kutoka nchini Kenya kwa kile alichozungumza.

Akifanyiwa mahojiano na mtangazaji Millardayo Ben Pol alieleza kuwa hakuwahi kufurahia ndoa yake na Anerlisa.

Baada ya mahojiano hayo Anerlisa alimuomba Ben Pol aache kumzungumzia na akaahidi endapo ataendelea basi atapost meseji zake kwani anqchoongea kwenye media ni tofauti na anachomtumia.

Sasa  kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa lengo lake lilikuwa kueleza namna alivyopitia magumu na kuathirika kisaikolojia hakuwa na lengo na kumuumiza aliyekuwa mke wake Arnelisa.

Ben Pol amechukua hatua hiyo mara baada ya Arnelisa kuanika hadharani meseji ambazo msanii huyo alikuwa akimtumia kupitia WhatsApp akitaka warudiane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *