Entertainment

BEYONCE KUTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA OSCAR JUMAPILI HII

BEYONCE KUTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA OSCAR JUMAPILI HII

Mwanamuziki maarufu duniani Beyonce ametajwa kutumbuiza kwenye tuzo za 94 za Oscar zitakazofanyika, Machi 27 katika ukumbi wa Dolby Thearter,nchini Marekani.

Beyonce anatajwa kutumbuiza wimbo “Be alive” ambao unapatikana kwenye filamu ya King Richard. Wasanii wengine ambao wanatarajiwa kuwasha moto kwenye jukwaa hilo ni pamoja Van Morrison wimbo “Down to joy”, ambao unatikana kwenye filamu ya Belfast, wengine ni Billie Eilish & Finneas ambao watatumbuiza wimbo “No time to die” unayopatikana kwenye filamu ya No time to die, na wasanii wengine wengi.

Tuzo hizo maarufu za filamu duniani, zitahudhuriwa na mastaa kibao kutoka Marekani na nje ya Marekani. Tuzo hizo zina jumla ya vipengele 24 ambazo wasanii mbalimbali wakiwemo wa muziki na filamu wanaziwania.

Wakati huo huo Regina Hall, Amy Schumer na Wanda Sykes wanatarajiwa kuwa host wa tuzo hizo. Hii inakuwa kwa mara ya pili tangu mwaka 2011 tuzo hizo kuwa na host watatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *