Entertainment

Bien Amaliza Ugomvi wake na Otile Brown

Bien Amaliza Ugomvi wake na Otile Brown

Msanii Bien Baraza kutoka Kenya, ametangaza kuwa tofauti zake na mwimbaji Otile Brown sasa zimefikia mwisho, na wawili hao wako katika uhusiano mzuri.

Akizungumza kwenye mahhojiano kupitia Mic Cheque Podcast, Bien amesema kuwa wamezungumza na kusameheana baada ya kipindi cha kutokuelewana kilichodumu kwa muda.

Bien amefichua kuwa wakati wa mzozo wao, Otile aliuchukulia suala hilo kwa uzito kiasi cha kumzuia (Block) kwenye mitandao ya kijamii, hatua iliyokuwa ishara ya sintofahamu iliyotanda kati yao

Bien amempongeza Otile kwa juhudi na kazi yake kwenye muziki, akieleza kuwa licha ya tofauti zao, amekuwa akimthamini kama msanii mwenye nidhamu na bidii ya kazi.

Mashabiki wamepokea habari hii kwa furaha, wakitumai kuwa hatua hiyo inaweza kufungua milango ya ushirikiano wa kimuziki kati ya wasanii hao wawili maarufu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *