Mwanamuziki Bien Baraza ametangaza msanii chipukizi Original Stinger kuwa mshindi wa shindano lake la mtandaoni “All My Enemies Are Suffering Challenge”
Katika tangazo hilo, Bien ameeleza kuwa Original Stinger alishinda kutokana na ubunifu, utofauti na kiwango cha juu cha utendaji katika kazi yake, ambacho kilimtofautisha na washiriki wengine wengi waliokuwa wamejitokeza.
Bien amemzawadia mshindi huyo kiasi cha KSh130,000, kama motisha kwa kazi yake na kama sehemu ya juhudi za kuunga mkono vipaji vipya katika muziki wa Kenya. Ametoa pia shukrani zake kwa washiriki wote waliojitokeza, akisema kuwa ubunifu ulioonekana katika shindano hilo unaonyesha ukuaji mkubwa wa tasnia ya muziki Afrika Mashariki.
Kupitia shindano hilo, wasanii walihimizwa kuonyesha ubunifu wao kwa kutumia wimbo wa Bien, na mamia ya vijana walituma kazi zao kwa matumaini ya kushinda. Original Stinger alitajwa kuwa miongoni mwa walioleta delivery kali zaidi, sauti thabiti na ujumbe ulioendana na mahitaji ya shindano.