Entertainment

Bien Apongeza Kodong Klan kwa Onyesho la Lililouza Tiketi Zote Nairobi

Bien Apongeza Kodong Klan kwa Onyesho la Lililouza Tiketi Zote Nairobi

Msanii kutoka kundi la Sauti Sol, Bien Aime Baraza, amewapongeza wanamuziki wa Kodong Klan kwa mafanikio makubwa ya onyesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Masshouse Jijini Nairobi, ambapo tiketi zote ziliuzwa.

Katika ujumbe wake wa pongezi, Bien ameeleza kuwa onyesho hilo lilikuwa miongoni mwa maonyesho bora zaidi aliyowahi kushuhudia katika tasnia ya muziki, akisisitiza kuwa wasanii wa Kenya wameendelea kuthibitisha ubora wao katika sanaa ya muziki.

Mkali huyo wa ngoma ya My Enemies Are Suffering, amesema kwamba mashabiki walipata thamani ya pesa zao na hata kudokeza kuwa kiwango cha ubora kilichoonyeshwa kingestahili malipo ya juu zaidi.

Bien pia ameonyesha fahari yake kwa mafanikio ya Kodong Klan, akisema kundi hilo limejenga msingi imara katika tasnia ya muziki wa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *