Entertainment

Bien Atajwa Kutumbuiza Afro Nation Portugal 2026

Bien Atajwa Kutumbuiza Afro Nation Portugal 2026

Mwanamuziki wa Kenya, Bien-Aimé Baraza, amepata mafanikio makubwa baada ya kutangazwa rasmi kuwa miongoni mwa mastaa watakaotumbuiza kwenye tamasha kubwa la kimataifa la Afro Nation Portugal 2026.

Tamasha hilo, linalotajwa kuwa moja ya makubwa zaidi duniani kwa muziki wa Afrobeats na muziki wa Kiafrika, litafanyika kuanzia Julai 3 hadi 5 katika jiji la Portimão, Algarve nchini Ureno.

Bien atapanda jukwaa moja na majina makubwa duniani akiwemo Wizkid, Asake, Tyla, Gunna, Mariah the Scientist, na Olamide, miongoni mwa wengine. Uwepo wake katika orodha hii unatajwa kama ushindi mkubwa kwa muziki wa Kenya na uthibitisho wa nafasi ya wasanii wa Afrika Mashariki katika ramani ya muziki wa kimataifa.

Afro Nation Portugal, tangu kuanzishwa kwake, limekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa muziki kutoka kote ulimwenguni, likijulikana kwa kukutanisha wakali wa Afrobeat, Amapiano, Dancehall na Hip Hop kwenye jukwaa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *