Entertainment

Bien Atimiza Ahadi ya Kshs 130,000 kwa Mshindi wa All My Enemies Are Suffering Challange

Bien Atimiza Ahadi ya Kshs 130,000 kwa Mshindi wa All My Enemies Are Suffering Challange

Msanii wa Sauti Sol, Bien-Aimé Baraza, amemkabidhi rasmi rapper Original Stinger KSh130,000 baada ya kumtangaza mshindi wa “All My Enemies Are Suffering” Challenge, shindano lililovutia mamia ya vijana wanaochipukia katika muziki.

Akizungumza alipokabidhi fedha hizo, Bien amemsifu Stinger kwa kufanya kazi yake kwa bidii na kumpongeza kwa kutumia muziki kama nguzo ya kujikwamua na kujiendeleza. Ameongeza kuwa shindano hilo lililenga kuwapa nafasi wasanii chipukizi kuonyesha uwezo wao na kupata kutambulika katika tasnia ya muziki.

Original Stinger, kwa upande wake, ameonyesha shukrani kwa Bien na mashabiki wote waliomuunga mkono, akisema kuwa ushindi huo umempa nguvu mpya ya kuendelea kutengeneza muziki wenye ubora na kusukuma brand yake mbele zaidi.

Tuzo hiyo ilitolewa mbele ya mashabiki katika hafla maalum iliyoandaliwa kwa heshima ya DJ AG kutoka Uingereza ambaye kwa sasa yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *