
Msanii wa Sauti Sol, Bien amedai kwamba anaunga mkono harakati za mchekeshaji Eric Omondi kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya muziki nchini.
Katika mahojiano na Plug tv, Bien amesema kitu ambacho kinamfanya wakati mwingine kutofautiana kimawazo na Eric Omondi ni kutokana na mchekeshaji huyo kuingiza kiki nyingi kwenye masuala muhimu.
Bien amesema licha ya kwamba wamekuwa wakitupia maneno makali mtandaoni na Eric Omondi, anaheshimu kila ambacho mchekeshaji huyo anakifanya kwa kuwa anajituma sana kwenye shughuli zinazomuingizia kipato.
Katika hatua nyingine Bien amewataka wakenya waache kasumba ya kuwashambulia watengeneza maudhui na badala yake wawe mstari wa mbele kuunga mkono shughuli zao kwani kuwakosa kila mara ni ulimbukeni wa hali ya juu.