Entertainment

Bien Azindua Rasmi Shindano la Open Verse Duniani

Bien Azindua Rasmi Shindano la Open Verse Duniani

Msanii nyota wa Kenya, Bien, ameanzisha rasmi shindano la Open Verse Challenge kupitia wimbo wake maarufu “All My Enemies Are Suffering.”

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bien ametoa mwaliko kwa wasanii na wabunifu kutoka kote duniani kushiriki kwa kurekodi remix ya wimbo huo na kuonyesha ubunifu wao. Mshindi ataondoka na zawadi ya dola 1,000 za Kimarekani (takribani Shilingi 130,000 za Kenya).

Bien amesema kuwa shindano hili limefunguliwa kwa kila mtu duniani na litafungwa mnamo tarehe 7 Novemba 2025. Washiriki wanatakiwa kupakia remix zao kwenye mitandao ya kijamii, kumtag Bien, na kutumia alama ya reli #AllMyEnemiesChallenge.

Bien pia amefichua kuwa wakali wa muziki Khaligraph Jones (kutoka Afrika Mashariki) na rapa wa Nigeria Phyno (kutoka Afrika Magharibi) wanalifuatilia kwa karibu shindano hili.

“Phyno alileta ladha ya Naija, sasa ni zamu yenu,” alisema Bien akiwatia moyo vipaji vipya.

Kwa ushiriki wa majina makubwa ya muziki kutoka Mashariki na Magharibi mwa Afrika, mashabiki na wasanii chipukizi wanasubiri kwa hamu kuona ni nani atakayeibuka kidedea katika shindano hili linalotarajiwa kuwa kali zaidi mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *