Vita vya maneno kati ya VJ Patelo na rapa Toxic Lyrikali vimechacha tena mtandaoni, safari hii vikihusisha majigambo ya fedha na vito vya thamani.
Toxic Lyrikali ndiye alianza mashambulizi kupitia Instagram Live kwa kudai kuwa Patelo anaishi kwa kutegemea pesa za mke wake, Dee, jambo lililozua mjadala mkali kati ya mashabiki wao.
Hata hivyo, Patelo hakusita kujibu. Kupitia mitandao ya kijamii, ameonyesha maisha yake ya kifahari na misururu ya minyororo ya thamani, huku akimkejeli Toxic kwa kusema kuwa minyororo yake ni “miyoo” (bandia).
Mashabiki wa pande zote mbili wameendelea kutoa maoni tofauti, wengine wakimtetea Patelo kwa kudai anajitegemea, huku wengine wakisema Toxic Lyrikali alikuwa anasema ukweli kuhusu maisha ya VJ huyo. Vita hivyo vya maneno vinaonekana kuendelea, huku kila upande ukijaribu kuthibitisha nani ni “boss” halisi katika maisha ya kifahari.