
Msanii aliyegeukia siasa Bobi Wine amedai kuwa hana upendeleo kwa mgombea yeyote wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA kwa kuwa wote ni marafiki zake.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Bobi Wine amesema wasanii kuwa na chama chao sio kitu kibaya ila serikali inatumia chama cha UMA kuwatengenisha wasanii kwa misingi ya kiasasa.
Bobi Wine serikali haina nia ya kuboresha tasnia ya muziki, hivyo imeamua kuwahujumu wasanii ili kusiwahi tokea mtu kama yeye ambaye anatetea haki za wananchi kutoka udhalimu wa watu walio madarakani.
Kauli ya Bobi Wine imekuja mara baada ya kuonekana kuegemea upande wa King Saha alipoidhinishwa kugombea urais wa chama cha wanamuziki Uganda uma kwa kutia saini fomu ya kuteuliwa kwake.
Ikumbukwe inaripoti kuwa Cindy Sanyu ambaye anagombea urais wa uma ana uhusiano mzuri na serikali ya Yoweri Museveni huku King Saha akionekana kuwa upande wa upinzani unaoongozwa na Bobi Wine.