Entertainment

Boomplay Kenya yataja wasanii waliosikilizwa zaidi mwaka 2022

Boomplay Kenya yataja wasanii waliosikilizwa zaidi mwaka 2022

Katika kufunga mwaka kwenye tasnia ya muziki nchini, App namba moja kwenye utoaji wa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, Boomplay, imetoa takwimu zake za kila mwaka, “Boomplay Recap 2022”.

Boomplay music Kenya imewataja wanamuziki watatu wa kiume na wakike walioongoza kwa kusikilizwa mwaka huu kwenye App hiyo.

Kwa mujibu wa Boomplay wanamuziki hao ni Otile Brown, Bahati na Wakadinali kwa kuzingatia idadi zao za streams kuanzia tarehe 1/11/2021 hadi 30/10/2022.

Kwa upande wa wasanii wa Kike,Nadia Mukami anaongoza orodha hiyo akifuatwa na Mercy Masika huku Nikita Kering akifunga tatu bora.

Lakini pia Boomplay imewataja wanamuziki wa Kenya walioshamiri zaidi kwa mwaka 2022 ambao wamekuwa na mwaka mzuri wa ukuaji. Wasanii hao ni pamoja na Iyanii, Fathermoh na Nasha Travis.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *