Entertainment

BOSI WA TOP DAWG AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA KENDRICK LAMAR

BOSI WA TOP DAWG AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA KENDRICK LAMAR

Rais wa Top Dawg Entertainment, Terrence “Punch” Henderson amesema bado anajali kuhusu maendeleo ya rapa Kendrick Lamar licha ya kuachana na Label hiyo mwaka huu.

Akizungumza na podcast ya My Expert Opinion Punch amesema “Ninajali kuhusu yeye kiujumla kama binadamu. Ni kama kutumia mfano wa mtoto, kuna wakati wataenda nje, huwezi kwenda nao kila wanapoenda. Wataenda nje na kutafuta uzoefu.” huku akikazia kwamba, hata akikwama basi asisite kumpigia simu kwa ushauri.

Utakumbuka Kendrick Lamar aliondoka kwenye Label ya Top Dawg Entertainment ambayo aliitumikia kwa takriban miaka 17 punde tu baada ya kuachia album yake Mr. Morale and the Big Steppers.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *