Entertainment

Boutross Atetea Wasanii wa Kenya Kushiriki Event za Serikali

Boutross Atetea Wasanii wa Kenya Kushiriki Event za Serikali

Msanii wa muziki wa hip hop, Boutross Munene, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mjadala unaoendelea wa wasanii kutumbuiza kwenye hafla zinazohusishwa na serikali.

Akipiga stori na Iko Nini Podcast, rapa huyo amesema kuwa hatowahi kuacha kutafuta kazi kwa sababu ya mivutano ya kisiasa kwa kuwa hatashindwa kujikimu kimaisha.

Kwa mujibu wake, uaminifu wake uko kwenye sanaa na kipato cha maisha, na si kwenye mrengo wowote wa kisiasa kama namna baadhi ya watu waanavyodai.

Rapa huyo amefafanua kuwa hana pingamizi kutumbuiza kwenye uzinduzi wa matatu wa George Ruto au tukio lolote la kisiasa, akisisitiza kuwa kila jukwaa ni nafasi ya kuonesha kipaji na kupata riziki.

Aidha, ameongeza kuwa umati unaohudhuria hafla kama hizo ni uthibitisho tosha kwamba Wakenya bado wanapenda kuona wasanii wakitumbuiza bila kujali mazingira ya kisiasa.

Hata hivyo amewataka wakenya kuwaunga wasanii wao bila kuwawekea vikwazo vya kisiasa kwani wasanii wengi wanategemea muziki wao kama kitega uchumi.

Kauli ya Boutross imeibua mjadala mpana mitandaoni, huku mashabiki na wachambuzi wakitofautiana kuhusu nafasi ya wasanii katika matukio yenye msukumo wa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *