Entertainment

BOW BOW ATANGAZA KUACHIA ALBUM YAKE MWISHO CHINI YA DEATH ROW INAYOMILIKIWA NA SNOOP DOGG

BOW BOW ATANGAZA KUACHIA ALBUM YAKE MWISHO CHINI YA DEATH ROW INAYOMILIKIWA NA SNOOP DOGG

Rapa kutoka nchini Marekani Bow Wow ambaye juzi kati alitangaza kuachana Muziki, ameurudi kule ambako safari yake ilianzia, ambapo ni mikononi mwa rapa Snoop Dogg ambaye aligundua kipaji chake akiwa na umri wa miaka 6.

Kupitia ukurasa wake Twitter Bow Wow ametusanua kuwa album yake ya mwisho kwenye muziki ‘Before 30’ itatoka chini ya lebo ya muziki ya Death Row Records ambayo hivi karibuni ilipata mmiliki mpya ambaye ni Snoop Dogg.

Bow Wow anastaafu muziki huku akiwa na majuto moyoni, mapema mwaka huu alifunguka kuwa anajutia kufanya muziki katika maisha yake na ni heri angekuwa anafanya uigizaji pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *