Sports news

Brazil yatupwa nje Kombe la Dunia

Brazil yatupwa nje Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Croatia imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa kuiondosha Brazil kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya 1-1

Brazil ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo kabla ya kukutana na kigingi cha Croatia walioendeleza kile walichokifanya kwenye fainali zilizopita walipovuka kwenye hatua zote za mtoano kwa kucheza dakika 120 kuanzia hatua ya 16 Bora hadi fainali walipofungwa na Ufaransa

Mwaka huu Croatia imewatoa Japan katika hatua ya 16 Bora na sasa wamewaondosha Brazil kwa mbinu zile zile na watakutana Argentina kwenye nusu fainali

Argentina ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa kuwaondosha Uholanzi kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya 2-2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *