Msanii anayesuasua kimuziki nchini Kenya, Brown Mauzo, ameanza ukurasa mpya wa maisha baada ya kufunga ndoa rasmi na mpenzi wake mpya, mwaka mmoja tu tangu kuvunja ndoa yake na socialite maarufu nchini humo Vera Sidika.
Kupitia mitandao ya kijamii, Mauzo amepakia misururu ya picha za harusi yake, akionyesha furaha na shukrani kwa hatua hiyo muhimu maishani mwake. Hata hivyo, ameamua kuficha uso wa mke wake mpya, hatua iliyozua gumzo miongoni mwa mashabiki na kufufua hamu ya kutaka kumjua mrembo huyo.
Brown Mauzo hajatoa maelezo zaidi kuhusu harusi hiyo wala utambulisho wa mke wake, lakini ujumbe wake Mtandaoni unaashiria kuwa yuko kwenye kipindi kipya cha amani, furaha na faragha.