
Msanii Brown Mauzo, ametangaza rasmi kwamba atawania kiti cha Mjumbe wa Wadi (MCA) wa Kileleshwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Kupitia ujumbe wake kwa wakazi wa Kileleshwa, Mauzo amesema kuwa uamuzi wake umetokana na maombi na ushauri kutoka kwa jamii ambayo amekuwa akiishi nayo. Amesisitiza kuwa sauti ya wananchi wa Kileleshwa ndio imekuwa ikimpa motisha ya kuingia katika siasa.
Mauzo ambaye pia ni mume wa zamani wa socialite Vera Sidika, ameongeza kuwa yuko tayari kushirikiana na wakazi wa Kileleshwa kubadilisha ward hiyo na kuboresha maisha ya watu.
Hata hivyo, ameshukuru kwa imani na kuungwa mkono na wananchi, akiahidi kuendesha uongozi wa karibu na wananchi na unaolenga maendeleo.