Gossip

Brown Mauzo Aweka Mipaka ya Simu Usiku kwa Wazazi Wenza

Brown Mauzo Aweka Mipaka ya Simu Usiku kwa Wazazi Wenza

Mwanamuziki wa Kenya Brown Mauzo ameweka wazi msimamo wake kuhusu mawasiliano katika mpangilio wa malezi ya pamoja (co-parenting), akisema hatakubali kupokea simu za usiku wa manane isipokuwa pale ambapo kuna dharura ya kweli.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mitandaoni, Mauzo ameeleza kuwa anathamini mipaka na utaratibu wa mawasiliano katika malezi ya watoto, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana kati ya wazazi wanaoshirikiana kulea.

Mauzo, ambaye amekuwa akihusiana na mijadala ya malezi ya pamoja kwenye mitandao, amesema anataka kuhakikisha mawasiliano yanabaki ya heshima na yanafaa kwa maslahi ya watoto.

Hata hivyo, haijabainika iwapo kauli hiyo ilimlenga Vera Sidika ila walimwengu mitandaoni wamehoji kuwa huenda kuna mgogoro ambao umeibuka kati yake na Baby Mama wake huyo ambaye kwa muda wamekuwa wakishirikiana kwenye safari ya ulezi wa pamoja.

Kauli yake imezua mjadala miongoni mwa mashabiki na wafuasi, huku baadhi wakimuunga mkono kwa kuweka mipaka, na wengine wakihisi kuwa ujumbe huo ulilengwa kwa mtu maalum.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *