Entertainment

Bruce Melody aachia Album yake mpya Colorful Generation

Bruce Melody aachia Album yake mpya Colorful Generation

Mwanamuziki maarufu nchini Rwanda, Bruce Melodie, ameachia albamu yake mpya Colorful Generation. Albamu hii ina nyimbo 21 na inajumuisha mchanganyiko wa Afropop, Amapiano, na R&B, ikiwa na kolabo na wasanii kama Joeboy, Blaq Diamond, Bien na Bensoul.

Nyimbo maarufu kwenye albamu ni “Beauty on Fire” akiwa na Joeboy, na “Niki Minaji” na Blaq Diamond, ambayo imejipatia umaarufu barani Afrika. Bruce Melodie, ambaye anajulikana kwa nyimbo kama Katerina na Bado, anaendelea kukuza umaarufu wake kimataifa baada ya kushinda Trace Awards 2023 kupitia kipengele cha Msanii Bora wa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *