Entertainment

BRUNO K AMCHANA CINDY SANYU KWA KUSHINDWA KUWATETEA WASANII

BRUNO K AMCHANA CINDY SANYU KWA KUSHINDWA KUWATETEA WASANII
Mwanamuziki kutoka nchini uganda Bruno K amemtolea uvivu msanii mwenzake Cindy Sanyu hii ni baada ya msanii huyo kudai kwamba Bruno K alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Black markert Records bila kuelewa mkataba wenyewe.
 
Akiwa kwenye moja ya interview Bruno K amesema madai ya Cindy ambaye ni rais wa chama cha wanamuziki nchini Uganda hayana msingi wote wote kwani kauli yake hiyo inaonyesha ni jinsi gani ameshindwa kuwatetea wasanii wanaonyanyaswa na lebo za muziki.
 
Bruno K kwa sasa anaendelea kushinikiza lebo ya muziki ya Black Market records impe channel yake ya youtube baada ya lebo hiyo kuchukua akaunti yake hiyo alipoigura lebo ya muziki ya Black Market  records.
 
Ikumbukwe juzi kati Cindy Sanyu aliwataka wasanii nchini uganda kuwa makini wanapotia sahihi mikataba na lebo za muziki kwani wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo bila kuwashirikisha mawakili.
 
 
 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *