
Staa wa muziki kutoka Nigeria Burna Boy ametajwa tena kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la Muziki nchini Marekani Coachella mwaka 2023.
Burna Boy ametajwa kwenye orodha ya wasanii ambao watatumbuiza Aprili 14 pamoja na wakali Bad Bunny, Pusha T, Becky G, Metro Boomin na wengine.
Tamasha hilo ambalo huenda kwa wikendi mbili, mwaka huu litaongozwa wakali kama Calvin Harris, Frank Ocean, Blackpink na Bad Bunny.
Hii inakuwa mara ya pili kwa Burna Boy kutumbuiza kwenye jukwaa kuu la tamasha hilo.