
Staa wa muziki kutoka Nigeria Burna Boy ametangaza rasmi kuachia album yake ya sita baada ya kupata mafanikio makubwa na album ya ‘Twice as Tall’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2020.
Akizungumza na mchekeshaji Trevor Noah kwenye, Burna boy amesema ataachia album yake mpya kwenye siku ya kuzaliwa kwake Julai 2 mwaka huu.
Ikumbukwe, Burna Boy kwa sasa yupo Jijini New York Marekani kwa ajili ya tour yake ya “Space Drift” ambapo anatarajia kufanya show yake leo kwenye ukumbi wa ‘Madison Square Garden’ ambao unaingiza watu elfu 20 huku akiwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kufanya show kwenye ukumbi huo.