Entertainment

Butita Amkingia Kifua Flaqo Kufuatia Skit Yenye Utata

Butita Amkingia Kifua Flaqo Kufuatia Skit Yenye Utata

Mchekeshaji na mtayarishaji wa maudhui nchini Kenya, Eddie Butita, amejiunga na mjadala ulioibuka kufuatia skiti ya hivi karibuni ya Flaqo inayodaiwa kuwalenga wafanyi biashara wa forex wanaodaiwa kuwa utajiri wao unatokana na biashara ya ushoga au mahusiano ya jinsia moja.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Butita alisisitiza kuwa katika skiti hiyo, Flaqo hakumtaja mtu yeyote moja kwa moja, jambo linalomfanya ashangae ni kwa nini baadhi ya watu wanajihisi kushambuliwa ikiwa kweli hawahusiki na masuala yaliyoigizwa. Aliongeza kuwa sanaa na ucheshi huwa na jukumu la kuibua mijadala na kutoa nafasi ya jamii kujitazama kwenye kioo.

Skiti hiyo ya Flaqo imezua mjadala mkali mitandaoni, ambapo baadhi ya wafuasi wake wamejitokeza kumtetea wakisema ni kazi ya kisanii inayotumia kejeli na utani kufichua uhalisia wa maisha, huku wakosoaji wakidai kuwa kugusia masuala yenye utata kama biashara ya “Sim2” au Ushoga ni kukiuka maadili na heshima, na kwamba inaweza kuathiri heshima ya sekta nyingine kama forex trading.

Mjadala huu unaonekana kugawanya maoni ya umma, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa uhuru wa ubunifu na wengine wakitaka wasanii kuwa makini wanapogusia mada nyeti zinazoweza kuibua hisia kali katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *