
Rapa maarufu wa Marekani, Cardi B, amekutwa hana hatia katika kesi ya madai yaliyofunguliwa na mlinzi wake wa zamani wa usalama, Emani Ellis.
Ellis alikuwa amemshataki Cardi B kwa madai ya kumshambulia kwenye ofisi ya daktari wa wanawake huko Beverly Hills mwaka 2018. Mlinzi huyo alidai Cardi alimshambulia, kumtemea mate, na kumtolea maneno ya ubaguzi wa rangi, na kuomba fidia ya $24 milioni (takriban Ksh bilioni 3.1).
Hata hivyo, ushahidi uliotolewa na mashahidi waliokuwa kliniki hiyo ulikanusha madai ya Ellis. Majaji wakachunguza ushahidi huu na hatimaye wakamua kusimama na Cardi B, wakimkuta hana hatia.
Akizungumza nje ya mahakama, Cardi B amesema kuwa atapambana na mtu yeyote atakayefungua shauri la uongo dhidi yake, akionya kuwa safari hii mhusika atalazimika kugharamia uharibifu wowote atakaomsababisha. Cardi B pia alisisitiza kuwa kesi hii ilikuwa njama ya kutaka pesa, na alieleza kuwa hana hofu ya kudai haki yake mbele ya sheria.
Uamuzi huu unamruhusu Cardi B kuendelea na maisha yake bila kuingiliwa na masuala ya kisheria yanayohusiana na tukio hilo la zamani, huku akiwakilisha mfano wa kushikilia haki binafsi na usalama wa heshima.