
Rapa Cardi B ataikata kiu yako ya muziki muda wowote kuanzia sasa baada ya ukimya wa miaka minne.
Rapa huyo kutoka nchini Marekani ameonekana akiwa studio kwenye picha ambayo imesambaa kwenye mitandao leo.
Mbali na picha hiyo, Cardi B ameifuata (follow) akaunti mpya iitwayo (Albumcb2) na kuashiria huenda ni ujio wa Album ya pili.
Cardi B alitubariki na Album yake ya kwanza ‘Invasion of Privacy’ mwaka 2018 na hadi leo amekuwa akitutia kiu kikali kwa kuachia kazi kwa manati.