
Mwanamuziki Catherine Kusasira aliuza gari lake aina ya Toyota Land cruiser V8 ambalo alizawadiwa na rais Yoweri Museveni.
Inadaiwa kuwa mwanamama huyo aliuza gari lake kwa sababu alikuwa anaandamwa na madeni.
Sasa akiwa kwenye moja ya interview Catherine Kusasira amejitokeza na kukanusha madai kuwa aliuza gari lake kutokana na madeni.
Hitmaker huyo “I love you” amesisitiza kwamba alipiga mnada gari Β lake kwa sababu watu wake wa karibu walikuwa wanamuonea wivu.
Mwimbaji huyo wa zamani wa lebo ya muziki ya Eagles productions amedai kuwa kuna baadhi ya watu waliibua madai hayo kumuaharibia jina kwa sababu anamuunga mkono Rais Museveni.
Hata hivyo Amethibitisha kuwa tayari ameagiza Β gari jipya aina toyota SUV ambayo haitawafanya watu wawe na wivu